Maandamano makubwa yalifanyika jana katika Msikiti wa Othman bin Affan kusini mwa Cairo ambapo wananchi waliokuwa na hasira walilaani vikali mapinduzi dhidi ya Mursi. Kwingineko Chama cha Uhuru na Uadilifu ambacho ni tawi la kisiasa la Harakati ya Ikwanul Muslimin kimetoa wito wa kufanyika maandamano makubwa ya kitaifa kote Misri Ijumaa hii. Essam el-Erian, naibu mwenyekiti wa chama hicho amesema kuondolewa Mursi madarakani ni sawa na kubatilisha mafanikio ya mwamko wa mwaka 2011 uliomuondoa madarakani dikteta kibaraka Hosni Mubarak.
Misri ilikumbwa na machafuko baada ya Mursi kupinduliwa na jeshi mapema mwezi wa Julai. Karibu zaidi ya watu 1,000 waliuawa baada ya wanajeshi wa Misri kuwashambulia wafuasi wa Mursi ambao walikuwa wakiandamana kwa amani Agosti 14.
waandamaji nchini Misri |
No comments:
Post a Comment