Pages

Sunday 27 July 2014

SIKILIZA QASWIDA YA ARAFA 'SANJARI' AKIWAOMBEA NA KUWALILIA WAPALESTINA

Mwimbaji wa Qasida maarufu wa nchini Tanzania Arafa Abdillah 'Sanjari' amewaimbia Qaswida wananchi wa Palestina walio katika madhila makubwa ya maonevu kutoka kwa walowezi wa Kiyahudi wanaoendeleza mashambulizi ya kijeshi katika ukanda wa Gaza.

Katika Qaswida hiyo amewaombea dua ndugu hao wa Kipalestina Mwenyezi Mungu awanusuru na udhalimu wa Kiyahudi. 
Arafa anakuwa Mwimbaji wa kwanza kutoka Tanzania Kuimba Qaswida kuhusiana na Dhulma kubwa wanaofanyiwa Wapalestina.

Maneno yaliyomo katika Qaswida hiyo ni haya:

1. Ndugu zetu hao, Rabbi warehemu
   Sio peke yao, Na waisilamu
   Tunalia nao, Tu kila sehemu
   Inusuru leo, Inavuja damu

2. Mbona ulifanya, Hushindwi Dayyani
   Ulivyomkanya, Mbabe Qaruni
   Alijidanganya, Nae Firauni
   Ukamgawanya, Ukamwacha duni

3. Mwisho wa fitina, Mwisho wa uhuni
   Na palestina, Wanautamani
   Unavyowaona, Hawana amani
   Ila wapigana, Silaha imani.

Sikiliza hapo chini Qaswida hiyo:

No comments:

Post a Comment