Pages

Monday, 9 September 2013

MWANAUME ALIYEBADILI JINSIA ASILIMU, AOLEWA MKE WA PILI

Lucy Vallender wa Manor Road, Swindon  amekuwa muingereza wa kwanza aliyebadilisha jinsia na baadae kusilimu.Lucy ambaye jina lake la awali alikuwa akifahamika kama Laurens kabla ya kubadilisha maumbile yake kwa sasa ameolewa na  mwanaume wa kiislamu na kuwa mke wa pili wa mume huyo.
Lucy mwenye umri wa miaka 28,alifahamiana na mumewe huyo kupitia mtandao wa kutafutia wachumba (dating site) na baadae kuoana,alifanyiwa operesheni ya kubadili jinsia yake miaka mitatu iliyopita.Mumewe huyo hakuwahi kujua kama Lucy alikuwa mwanaume  miaka iliyopita.

Lucy anayefahamika kwa jina lake la sasa kama Layla na aliyepata mafunzo ya kijeshi kuanzia mwaka 2004 mpaka 2006,Kwa sasa anavaa hijabu kamili kila akitoka nje ya nyumba yake ,akionesha ulimwengu kwamba ameolewa.

Lucy aliyekuwa akipenda sana kufyatua risasi katika mafunzo yake ya kijeshi,tangu akiwa na umri wa miaka 10 alihisi na kutamani kuwa mwanamke.Mwaka 1998 akiwa na umri wa miaka 13 aliwaambia wazazi wake kwamba anataka kufanya mabadiliko ya jinsia yake."Familia yangu walipatwa na huzuni sana kwa sababu ilimaanisha wasingepata wajukuu,walichanganyikiwa sana na ndugu yangu Soren hatujazungumza kwa miaka saba mpaka sasa"

Anaendelea kusema, "Nilijaribu kufanya vitu vya ukakamavu,ili niweze kuondoa kuwaza tofauti lakini haikusaidia kwa sababu nilikuwa najaribu kuwa mtu ambaye kiuhalisia sikuwa hivyo"
Aliongeza, "nilijihisi tofauti na wengine kwa sababu nilivutiwa na wanaume". Katika kuondoa mawazo ya kupenda kuwa mwanamke anasema alifanya jitihada mbalimbali lakini ilishindikana. "Nilikwenda club na marafiki na nilikuwa nakunywa sana pombe" Pia katika jitihada yake ya kubaki katika maumbile na hisia za kiume alijaribu kuanzisha uhusiano na wanawake kadhaa.

Anasema, "katika miezi michache Nilikuwa na marafiki wengi wa kike lakini kamwe sikuwahi kuwa na mahusiano ya kimwili". Anaongeza kusema, "Kujiunga na mafunzo ya kijeshi ilikuwa ni jaribio langu la mwisho la kuwa mwanaume halisi lakini,ilishindikana baada ya miaka miwili,kwani nilihisi kuwa katika maumbile nisiostahiki".
Baada ya kutoka katika mafundisho ya kijeshi, Lucy alianza kuvaa mavazi ya kike na  kufanya mahusiano na wanaume.Akakuza nywele zake na kupata tiba ya vichocheo vya kike kabla ya kufanyiwa opereshe ya kubadili jinsia yake.

Kabla ya kuhama nyumbani kwao na kufanya maamuzi ya kumuona daktari kwa ajili ya kubadili jinsia yake,Lucy alimuelezea mpango huo mama yake. "Nilimwambia mama yangu,alishtushwa kiasi kwamba alishindwa kusema chochote". Baadae alikwenda hospitali na akamueleza daktari wake kwamba yupo katika umbile asilostahili."Nilikuwa na wasiwasi kwa mara ya kwanza na nilishindwa kutengeneza maneno ya kumwambia daktari,lakini nilimwambia nataka kuwa mwanamke,na alinambia sawa"

Katika mabadiliko makubwa mengine ya maisha yake, yalikuja septemba mwaka jana wakati alipoamua kutoka katika dini yake na kuwa muislamu.Anasema alivutiwa na uislamu kwa namna unavyohimiza,kujali na kuleta amani katika mafundisho yake kuliko dini nyingine."Nilikuwa na fikra juu ya jambo hilo(la kusilimu) kwa muda mrefu lakini ilikuwa kama mwiko kusilimu (kwa imani yake ya zamani)" alisema. Baada ya kusilimu anasema amepata mabadiliko makubwa katika nafsi yake. "Nilijisikia vizuri na nikawa na kitu cha kuamini (uislamu)na mwishowe nilihisi furaha na faraja ambayo sikuwahi kuipata katika maisha yangu"alisema.

Kabla ya kusilimu alizitafiti dini za budha na uyahudi,"Nilikuwa natafuta muelekeo sahihi wa maisha, naupenda (uislamu) ni mzuri na amani"kusilimu kwake kulikuja katika kipindi cha kiangazi kilichopita na aliolewa na Bwana Murad katika sherehe ndogo iliyofanyika huko London nyumbani kwa Murad.Akielezea mahusiano yake ya kindoa na mumewe anasema,"Nampenda, ni mkarimu na mtu mwenye maneno matamu,nilimuona mara mbili toka Tulipooana,wakati tulipofanya jimai"

Alipoulizwa je wakati bwana Murad anamuoa alikuwa akijua historia yake ya nyuma,alijibu kwa kusema, "sikumwambia kwamba nilibadili jinsia lakini lazima alikuwa na wasiwasi alipoona makovu yangu"
Hata hivyo Lucy ameingia katika matatizo na msikiti wake aliokuwa akiutumia wa Swindon, Wiltshire,ambapo wamemzuia kusali na wanawake wengine.Anasema amefanywa muhanga na waumini ambao walimuuliza historia yake na kisha kumzuia kwa sababu amebadili jinsia na kwamba hatakiwi kusali pamoja na wanawake kwani yeye ni mwanaume."Walisema nisisali na wanawake kwani mimi ni mwananaume,niliwaambia mimi ni mwanamke na nikaondoka zangu."

Pia amewalalamikia polisi kwa kutokuchukua hatua zozote kwa kubaguliwa kwake.Kwa sasa Lucy anataka kujua haki yake juu ya hukumu ya mtu aliyebadili jinsia katika uislamu.Aidha analalamikia waumini kwamba wanamchukulia katika namna isiyopendeza na kumnyanyapaa, "Wananiuliza maswali kuhusu saizi ya sidiria ninayovaa,kuhusu ukubwa wa koromelo,siku zangu za hedhi,na kutaka kuona cheti changu cha kuzaliwa" alilalamika na kuongeza, "Natumaini watu watabadili mienendo yao ili watu wengine kama mimi tuweze kuwa huru".Ingawa hasali katika msikiti huo, anaendelea kufanya ibada nyumbani kwake na anajifunza masuala mbalimbali ya dini na Quran.

Akizungumzia madai ya Lucy kuzuiwa kusali,msemaji wa msikiti huo amesema hajazuiwa kusali bali asali sehemu ya wanaume na si vinginevyo.Alisema, "Layla alijiunga katika darsa letu la kinamama mwishoni mwa mwaka jana,kwa nia ya kujifunza kiarabu."
"Hakuwa anajua kabisa kiarabu wakati anajiunga na darsa letu lakini miezi michache alikuwa na maendeleo mazuri.Alishirikiana na wana darsa na wanawake wote mpaka alipoondoka mwezi Juni mwaka huu,hatukujua kama alifanya mabadiliko ya jinsia."

Msemaji huyo aliongeza Kwamba Layla hakuweka wazi mabadiliko ya jinsia yake wakati wa kujaza fomu ya kujiunga na darsa.Na walianza kuhisi kuna anachoficha baada ya kutaka kuolewa kwani hakuonesha furaha pale alipotakiwa kuwasilisha vielelezo vya utambulisho wake. "Kwa bahati mbaya,hakuwa na furaha ya kuwasilisha hati yake kama vile pasipoti au cheti cha kuzaliwa kama sehemu ya mchakato wa ndoa yake" aliongeza msemaji huyo.

Anasema Layla hukuweza kufanya hivyo na badala yake akatumia njia ya kulalamika kwamba mwalimu wake wa kujitolea amemnyanyasa kwa kumuuliza maswali ya kumdhalilisha kama siku zake za hedhi na ukubwa wa matiti yake, na baada ya darsa Layla alimtumia mwalimu wake meseji za vitisho.Baadae palifanyika kikao na mwisho Layla aliomba msamaha na kusema anaondoka kwenda London kwa ajili ya kuolewa.Layla alisema kwamba cheti au pasipoti si muhimu katika ndoa ya kiislamu na kwamba msikiti hauna haki ya kuthibitisha kama yeye ni mwanamke au mwanaume
Lucy ambaye alifanyiwa operesheni huko London, pia aliwahi kufanya kazi katika wizara ya ulinzi kama mbeba mizigo ya jikoni.

Habari kwa hisani ya ahbaabur.blogspot.com



Lucy kushoto akiwa na kaka yake Soren (aliye kulia)

Msikiti wa swindon alipokuwa akisali


No comments:

Post a Comment