Shadi Hamid ameviambia vyombo vya habari vya Misri kwamba Rais Barack Obama ni mwanachama wa Ikhwanul muslimin kwa muda mrefu.Taarifa hiyo iliyokuja kwa njia ya Twitter na pia kupitia katika kurasa za mbele za magazeti ya Misri,imezua mjadala mkubwa kwa wafuatiliaji wa siasa za kimataifa.
Aidha Shadi alisema ndani ya habari hiyo kwamba Khairat al Shafer ambaye ni mtoto wa kiongonzi wa kikundi cha Ikhwanul Muslimin,aliwahi kumtisha Rais Obama wa Marekani kwamba atatoa nyaraka zinazoonyesha uwanachama wa Rais wa huyo katika kikundi cha Ikhwanul Muslimin. Taarifa hiyo inasema kwamba Obama alivutiwa na Ikhwanul Muslim wakati alipokuwa akiishi nchini Indonesia.
Ukiachana na tuhuma hizo zinazomkabili Rais Obama kuhusu uwanachama wake katika kikundi hicho,habari kwenye gazeti la Al-Wafd zimeeleza kwamba Malik Obama ambaye ni kaka wa rais Obama wa Marekani anahusishwa na uwanaharakati wa kikundi cha Al-Qaeda.
Wakati huo huo,Jonathan Spyer mwenye asili ya kiarabu ambaye ni kiongozi mwandaminzi wa kituo cha utafiti cha Global International Affears amelilalamikia gazeti la Al-Wafd kwamba ndilo ambalo limemtuhumu moja kwa moja rais Obama kuwa mwanachama wa Ikhwanul Muslimin.
Jonathan Spyer anaamini kwamba madai hayo yamejikita kwa kule kutokuridhishwa na sera za Obama pale alipo kataa kuelezea ukosolewaji wa Morsi na Chama chake cha Ikhwanul muslimin.Wote ambao hawamkubali Morsi na serikali yake iliyoondolewa madarakani na jeshi la nchi hiyo,wanamuona Obama ni mfuasi mzuri wa Morsi na Ikhwanul Muslimin.
Kwa mujibu wa Spyer anasema wamisri wanaamini Obama amekosa busara za kustaajabisha na tabia isiyo nzuri dhidi ya Ikhwanul Muslimin ambapo kwa dhati wanaamini kunasababishwa na hofu ya ufichuliwaji wa siri ya uanachama wake katika kikundi hicho.
Taarifa zinaelezea kwamba vyombo vya habari vya Misri havina mipaka linapokuja suala la ukosolewaji wa rais Obama wa Marekani.
Habari kwa hisani ya ahbaabur.blogspot.com
Gazeti la Al-Wafd la 30 august,2013 |
malik obama na barack obama,oktoba 3,1992.Katika harusi ya obama ambapo malik alikuwa bestman wa obama |
No comments:
Post a Comment