Pages

Wednesday 21 August 2013

OIC: ISRAEL ILAZIMISHWE KUHESHIMU MAENEO MATUKUFU

Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiislamu (OIC) umeitaka jamii ya kimataifa iilazimishe Israel kufuata sheria za kimataifa zinazoilazimisha kuheshimu maeneo ya kidini inayoyakalia kwa mabavu. OIC imesema hayo katika katika taarifa yake kwa mnasaba wa kutumia miaka 44 tangu Wazayuni walipochoma moto Msikiti mtukufu wa al Aqswa. 

Taarifa hiyo imeeleza kwamba, utawala wa Kizayuni wa Israel bado unaendelea kushambulia, kuharibu na kuvunjia heshima maeneo ya kidini ya Palestina inayoyakalia kwa mabavu ikiwemo Quds Tukufu. OIC sambamba na kuashiria kuongezeka harakati za Wazayuni wenye misimamo mikali zenye lengo la kuharibu Msikiti wa al Aqswa na  badala yake kujenga hekalu lao,

 imesema kwamba, Israel inafanya kila njama ili kuwafukuza wakazi wa Quds katika mji huo ili iukalie kikamilifu na kwamba suala hilo ni ukiukaji wa wazi wa kanuni na sheria za kimataifa.


No comments:

Post a Comment