Pages

Wednesday 4 September 2013

LADY GAGA ATOA WIMBO WA KUDHALILISHA VAZI LA HIJABU

Wimbo wa mwanamuziki wa POP wa kimarekani Stefani Joanne Angelina Germanotta 27, maarufu kama Lady Gaga umezua mtafaruku na kuwasha hasira za waislamu baada ya kuonekana unadhalilisha mavazi ya wanawake wa kiislam.Wimbo huo mpya ulioutambulishwa hivi karibuni unajulikana kwa jina la Burqa.

Burqa (برقع) ni vazi linalovaliwa na wanawake wa kiislam wakiwa katika mkusanyiko wa watu.Vazi hili ni maarufu sana kwa wanawake wa Afghanistan na ulaya.Na sasa limepata umaarufu sehemu malimbali duniani.Vazi la stara ni sheria kwa mwanamke wa kiislamu kwa mujibu wa Qurani Tukufu
Kutokana na hilo watu wamepinga wimbo huo wa msanii Lady Gaga kutokana na yale maisha  anayoishi msanii huyo.Kwamba maudhui ya wimbo yanaonekana yanadhalilisha wanawake wa kiislam kwa maneno yaliyomo katika wimbo wa msanii huyo.

Baadhi ya maneno yaliyokuwemo ndani ya wimbo huo yanasema 
" I'm not a wandering slave, I am a woman of choice
My veil is protection for the gorgeousness of my face, Do you wanna see me naked, lover?
Do you wanna peek underneath the cover? Enigma popstar is fun, she wear burqa for fashion
It's not a statement as much as just a move of passion”
Kwa tafsiri isiyo rasmi ni kwamba, "mimi si mtumwa ninayegaagaa, ni mwanamke mwenye kujielewa.
Hijabu yangu ni kinga ya urembo wa sura yangu,unataka kuniona nikiwa mtupu,mpenzi?
Unataka kufikia kilicho chini ya stara? Enigma nyota wa pop anachekesha. Anavaa hijabu kama fasheni,Siyo kufikisha ujumbe bali kutimiza matakwa yake”

Mwanamuziki huyo mwenye kupendelea kukaa wazi sehemu kubwa ya mwili wake,amejiwa juu na wanawake wa kiislamu kwa udhalilishaji wa vazi hilo tukufu.Aidha mwenyewe lady Gaga anasema amefanya hivyo ili kulitia nguvu vazi hilo kwa jamii.Hata hivyo amepingwa vikali na wanawake wa kiislamu wa nchini Pakistani kwa kuambiwa vazi hilo haliitaji kutangazwa kwani ni amri iliyotoka kwa mwenyezi Mungu kwa mwanamke wa kiislamu kuvaa kwa kustiri maungo yake.

Kwa kuthibitisha hilo walinukuu aya isemayo “Na waambie waislamu wanawake wainamishe macho yao, na wazilinde tupu zao wala wasidhihirishe viungo vyao,isipokuwa vinavyodhihirika( uso na vitanga vya mikono). Na waangushe shungi zao mpaka vifuani mwao,na wasioneshe mapambo yao ila kwa waume zao,au baba zao,au baba za waume (wakwe zao) au watoto wao,au wanawake wenzao………..”  Aya hiyo ipo katika Surat Nnur aya ya 31


Mwanamuziki huyo bado hajatoa video ya wimbo huo,ila amejitokeza hadharani akiwa amevaa vazi hilo huku akiachia wazi sehemu ya maungo yake.Vita dhidi ya uislamu imekuwa ikifanywa na watu mbalimbali duniani ambapo matokeo yake yamefanya watu wengi kuingia katika uislamu kinyume na matarajio ya wanaoupiga vita. Baadhi ya nchi za ulaya wamekuwa wakilipiga vita vazi hilo la Burqa.

Habari kwa hisani ya ahbaabur.blogspot.com
Lady Gaga

Lady Gaga


Mwanamke wa kiislamu

Wanawake wa kiislamu

No comments:

Post a Comment