Tukio hilo limekuja wakati serikali ya jimbo la Quebec
ikijiandaa kutangaza kupiga marufuku vazi la hijabu na vazi lolote lenye
kuashiria dini katika sehemu zote za kazi.
Damu hiyo ya nguruwe imepakazwa karibu na mlango wa
kuingilia katika msikiti huo pamoja na kuwekwa barua inayowapa onyo waumini wa msikiti huo
kuacha kujishughulisha na mambo yote ya dini yao Quebec au warudi makwao .
Aidha sehemu ya barua hiyo inasema "msikiti huu umebatizwa kwa damu halisi
ya nguruwe toka Quebec"
Chicoutimi ni moyo wa jimbo la Quebec ambapo inakadiriwa
kuwa na wakazi 158,000, na silimia 99 ya wakazi wake ni watu wenye asili ya Quebec
wanaoongea kifaransa wa madhehebu ya
katoliki.Asilimia iliyobaki ni waislamu na madhehebu mengine.Takwimu hiyo ni ya
sensa ya mwaka 2011.
Akizungumzia tukio hilo meya wa mji Saguenay Jean Tremblay,
amelaani kitendo hicho kwa kusema ni cha udhalilishaji na si cha kuungwa mkono
na pia hakiwakilishi mtazamo wa watu wa
mji wake dhidi ya waislamu.
Aidha ametahadharisha endapo serikali itawasilisha mezani muswada wa sheria
wa upigwaji marufuku mavazi yenye uwashiria wa dini ili kuchunga tamaduni ya watu wa
Quebec.Alisema kwamba mjadala kama huo
utachochea chuki na matukio mbalimbali ya udhalilishaji dhidi ya uislamu.
“hakuna shaka kwamba uwasilishaji wa mawazo hayo dhidi ya
kuukandamiza uislamu yataleta mtafukuru mkubwa.Kwa kutovaa alama yoyote ya
kidini sambamba na hijabu kutainua hisia za wa Quebec kupinga dini ukilinganisha
na hali ilivyo sasa,” aliongeza meya huyo wa mji wa Saguenay.
Wakati huo huo, wazalendo wahafidhina wanaiona serikali
haikuchukua hatua za kutosha katika kudhibiti mchanganyiko wa tamaduni(dini na
watu wasiokuwa wa Quebec) nyingine.
wahafidhina hao wa Quebec wanaiga mtindo wa kibaguzi wakundi la kihafidhina la kimarekani lisilotaka
waislamu nchini mwao.Suala la kuwapa hifadhi watu wachache wenye tamaduni
tofauti na asili husika limekuwa likichemka kwa muda mrefu jimboni humo.
Watu wa jimbo hilo wamekuwa hawataki kuona utamaduni tofauti
na wa kwao,ambapo mbali na kutaka kuwekwa sheria za kupiga marufuku vazi la
hijabu,serikali ya jimbo hilo imekubali kupitisha matumizi ya lugha ya
kifaransa kuwa lugha pekee itakayotumika jimboni humo.Mapendekezo hayo
yameungwa mkono na wakazi wengi wa jimbo hilo.
Tukio hilo tayari limeripotiwa polisi, na wameanza uchunguzi wa kubaini nani aliyehusika.Mpaka sasa hakuna
mtu yeyote au kikundi kilichodai kuhusika na tukio hilo.Kwa mujibu wa mafundisho ya uislamu nyama na damu ya nguruwe ni haramu kwa ushahidi wa suratil Maidah aya ya tatu inayosema, "mmeharamishiwa mzoga na damu na nyama ya nguruwe....."
Habari kwa hisani ya ahbaabur.blogspot.com
sehemu ya mbele ya msikiti iliyopakazwa damu ya Nguruwe |
msikiti uliopakazwa damu ya nguruwe |
No comments:
Post a Comment