Wanawake wa Kiislamu nchini Ufaransa wamefanya maandamano
kutetea vazi la stara ya Kiislamu la Hijabu. Maandamano hayo yalifanyika jana
katika eneo la Trappes huko kaskazini mwa nchi hiyo. Wanawake hao wa Kiislamu
wameandamana kulalamikia ongezeko la
mashambulio yanayotokana na chuki dhidi ya Uislamu
wanayofanyiwa wanawake wanaovaa hijabu na kupinga ushadidishaji wa sheria
zinazoweka mipaka ya uvaaji hijabu nchini Ufaransa. Maandamano hayo yalianzia
mbele ya msikiti wa eneo la Trappes hadi kwenye jengo la Manispaa ya eneo hilo.
Maandamano ya jana yamefanyika kufuatia mashambulio ya mara kwa mara dhidi ya
wanawake wa Kiislamu wanaovaa hijabu na kushindwa polisi kukabiliana na vitendo
hivyo katika mji huo wa Trappes.
Mbali na Polisi ya
Trappes kushindwa kukabiliana na mashambulio yanayofanywa dhidi ya wanawake wa
Kiislamu wanaovaa hijabu, inatuhumiwa pia kushirikiana na watu wenye chuki na
Uislamu katika kufanya vitendo vya kibaguzi na miamala miovu dhidi ya Waislamu.
No comments:
Post a Comment