Pages

Saturday, 31 August 2013

UPDATES: SHEIKH MUHAMMAD BAKAR ATOKA HOSPITALI, MESEJI YA MWISHO YA MWANAWE ABUUBAKAR YAACHA UJUMBE MZITO

Asubuhi ya jana jumamosi mwanazuoni mkubwa Afrika na mudir wa madrasatul Shamsul maarif ya Tanga, Sheikh Muhammad Bakar Al burhan ametolewa katika hospitali ya taifa ya Muhimbili.Sheikh ametolewa baada ya kupata nafuu kubwa pamoja na maendeleo mazuri ya afya yake.

Sheikh alikuwa amelazwa hospitalini hapo tangu siku ya jumanne wiki hii akitokea katika hospitali ya mkoa wa morogoro kufuatia ajali ya gari aliyoipata wilaya ya dumila mkoani morogoro.

Aidha kwa sasa Sheikh ametakiwa na madaktari wa MOI waliokuwa wakimtibia kupata muda zaidi wa kupumzika ili kuimarisha zaidi afya yake.

Majeruhi wengine waliopewa ruhusa wiki hii ni Mwalimu Mussa kunema na Kambi Salumu.Majeruhi Idd Issa Nori bado yupo hospitali ya Muhimbili wodi ya sewahaji akiendelea kupata matibabu zaidi.

Wakati huo huo imetolewa meseji ya mwisho ya marehemu Abubakar mtoto wa sheikh Muhammad Bakar,aliyoituma siku moja kabla hajafariki.Meseji hiyo aliituma muda wa saa nane za mchana,sawa na muda aliofariki siku iliyofuata.

Baadhi ya watu aliowatumia meseji hiyo ni Ustaadh Walid Alhad,imam wa msikiti wa kichangani pamoja na wanafunzi wenzake aliokuwa anasoma nao kwa Sheikh Alhad omar,Magomeni dar es salaam katika madrasatul Tadhwamun.

Meseji hiyo ambayo kama ilikuwa ikibashiri kifo chake yenye ujumbe mzito wenye kuhitaji kuzingatiwa ilisomeka hivi;

"A,aleykum Pendelea saana kuhudhuria ktk mazishi na usisimame mbali na kaburi kuwa jirani nalo ili uione thamani yetu inavyokuwa baada ya kufa maana ile nguo tunayovishwa huwezi kuivaa ktk uhai na tunaviringishwa kwenye mkeka si tena kitanda kizuri ulichokuwa unalalia kisha tunaingizwa kwenye kishimo kirefu (MWANANDANI) na tunafukiwa udongo juu,hivi thamani yetu iko wapi? mpaka tunashindwa kumuabudu aliyetuumba. Tatizo nini,muda hatuna? au tatizo ujana?

Kama ujana, vijana wangapi wanaotangulia mbele ya haki kabla ya wazee? kama ni mzee unangoja nini wakati uzee ni dalili ya ukomo wa umri wako? Ni vema tukajiandaa mapema kwa sababu safari ni lazima insha allah, mchana mwema"

Habari kwa ihsani ya ahbaabur.blogspot.com


Sheikh Muhammad Bakar Al burhan

Mwalimu Mussa Kunema

Marehemu Abuubakar



No comments:

Post a Comment