Rais mpya wa Mali Ibrahim Boubacar Keita ametoa wito kwa watu wote nchini humo kushikamana na misingi na thamani za Kiislamu ili kuleta umoja na maelewano ya kitaifa.
Akizungumza katika mji mkuu wa nchi hiyo Bamako kwa mara ya kwanza baada ya ushindi katika uchaguzi wa rais uliofanyika hivi karibuni, Keita alisema mambo atakayoyapa umuhimu ni utawala wa kisheria, kuliimarisha jeshi na kupambana na ufisadi.
Keita amesisitiza kuwa yeye atakuwa rais wa watu wote wa Mali na kwamba sasa hakuna haja tena ya uhasama baina ya makundi mbali mbali nchini humo. Ibrahim Boubacar Keita ambaye ataapishwa mwezi ujao wa Septemba amesema hivi sasa Mali inakabiliwa na changamoto nyingi ambazo zinaweza kutatuliwa tu kwa kutegemea thamani za Kiislamu na kuvumiliana.
Mgogoro wa Mali ulianza tarehe 22 Machi mwaka huu wakati wanajeshi waasi wakiongozwa na Amadou Sanogo walipofanya mapinduzi yaliyomng'oa madarakani Rais Amadou Toumani Toure kwa madai kuwa ameshindwa kuzima uasi kaskazini mwa nchi hiyo. Baada ya hapo waasi walichukua udhibiti wa eneo la kaskazini mwa nchi hiyo. Hivi sasa baada ya uchaguzi utulivu umerejea nchini humo.

No comments:
Post a Comment