Mwimbaji wa Qasida maarufu wa nchini Tanzania Arafa Abdillah 'Sanjari' amewaimbia Qaswida wananchi wa Palestina walio katika madhila makubwa ya maonevu kutoka kwa walowezi wa Kiyahudi wanaoendeleza mashambulizi ya kijeshi katika ukanda wa Gaza.
Katika Qaswida hiyo amewaombea dua ndugu hao wa Kipalestina Mwenyezi Mungu awanusuru na udhalimu wa Kiyahudi.
Arafa anakuwa Mwimbaji wa kwanza kutoka Tanzania Kuimba Qaswida kuhusiana na Dhulma kubwa wanaofanyiwa Wapalestina.
Maneno yaliyomo katika Qaswida hiyo ni haya:
1. Ndugu zetu hao, Rabbi warehemu
Sio peke yao, Na waisilamu
Tunalia nao, Tu kila sehemu
Inusuru leo, Inavuja damu
2. Mbona ulifanya, Hushindwi Dayyani
Ulivyomkanya, Mbabe Qaruni
Alijidanganya, Nae Firauni
Ukamgawanya, Ukamwacha duni
3. Mwisho wa fitina, Mwisho wa uhuni
Na palestina, Wanautamani
Unavyowaona, Hawana amani
Ila wapigana, Silaha imani.
Sikiliza hapo chini Qaswida hiyo:
Sunday, 27 July 2014
Tuesday, 26 November 2013
TAARIFA KWA WAPENZI NA WASHABIKI WA ARAFA SANJARI
Arafa Sanjari yupo katika dimbwi/kazi nzito ya kuandaa album mpya ya Qaswida ambayo itawajia inshaallah kwa namna itakayowaridhisha kiujumbe, uimbaji,video nzuri, na hata ustadi wa shows. japo kuwa kazi ni kubwa, yenye changamoto tele na kubwa ni support kukosekana au ndogo, kupitia ngazi tofauti tofauti.
Napenda kusema Allah atatia wepesi na tawfiiq hata kukamilika maazimia. Nimekuwa nikipata maombi na maswali kuhusu Album mpya na vipi kimya kimezidi mno? Jibu; Tuko pamoja naandaa na tutaendelea kupeana taarifa zaidi. Karibuni kwa ARAFA SANJARI.
Thursday, 10 October 2013
Sunday, 6 October 2013
Monday, 9 September 2013
MWANAUME ALIYEBADILI JINSIA ASILIMU, AOLEWA MKE WA PILI
Lucy Vallender wa Manor Road, Swindon amekuwa muingereza wa kwanza aliyebadilisha jinsia na baadae kusilimu.Lucy ambaye jina lake la awali alikuwa akifahamika kama Laurens kabla ya kubadilisha maumbile yake kwa sasa ameolewa na mwanaume wa kiislamu na kuwa mke wa pili wa mume huyo.
Lucy mwenye umri wa miaka 28,alifahamiana na mumewe huyo kupitia mtandao wa kutafutia wachumba (dating site) na baadae kuoana,alifanyiwa operesheni ya kubadili jinsia yake miaka mitatu iliyopita.Mumewe huyo hakuwahi kujua kama Lucy alikuwa mwanaume miaka iliyopita.
Lucy anayefahamika kwa jina lake la sasa kama Layla na aliyepata mafunzo ya kijeshi kuanzia mwaka 2004 mpaka 2006,Kwa sasa anavaa hijabu kamili kila akitoka nje ya nyumba yake ,akionesha ulimwengu kwamba ameolewa.
Lucy aliyekuwa akipenda sana kufyatua risasi katika mafunzo yake ya kijeshi,tangu akiwa na umri wa miaka 10 alihisi na kutamani kuwa mwanamke.Mwaka 1998 akiwa na umri wa miaka 13 aliwaambia wazazi wake kwamba anataka kufanya mabadiliko ya jinsia yake."Familia yangu walipatwa na huzuni sana kwa sababu ilimaanisha wasingepata wajukuu,walichanganyikiwa sana na ndugu yangu Soren hatujazungumza kwa miaka saba mpaka sasa"
Anaendelea kusema, "Nilijaribu kufanya vitu vya ukakamavu,ili niweze kuondoa kuwaza tofauti lakini haikusaidia kwa sababu nilikuwa najaribu kuwa mtu ambaye kiuhalisia sikuwa hivyo"
Aliongeza, "nilijihisi tofauti na wengine kwa sababu nilivutiwa na wanaume". Katika kuondoa mawazo ya kupenda kuwa mwanamke anasema alifanya jitihada mbalimbali lakini ilishindikana. "Nilikwenda club na marafiki na nilikuwa nakunywa sana pombe" Pia katika jitihada yake ya kubaki katika maumbile na hisia za kiume alijaribu kuanzisha uhusiano na wanawake kadhaa.
Anasema, "katika miezi michache Nilikuwa na marafiki wengi wa kike lakini kamwe sikuwahi kuwa na mahusiano ya kimwili". Anaongeza kusema, "Kujiunga na mafunzo ya kijeshi ilikuwa ni jaribio langu la mwisho la kuwa mwanaume halisi lakini,ilishindikana baada ya miaka miwili,kwani nilihisi kuwa katika maumbile nisiostahiki".
Baada ya kutoka katika mafundisho ya kijeshi, Lucy alianza kuvaa mavazi ya kike na kufanya mahusiano na wanaume.Akakuza nywele zake na kupata tiba ya vichocheo vya kike kabla ya kufanyiwa opereshe ya kubadili jinsia yake.
Kabla ya kuhama nyumbani kwao na kufanya maamuzi ya kumuona daktari kwa ajili ya kubadili jinsia yake,Lucy alimuelezea mpango huo mama yake. "Nilimwambia mama yangu,alishtushwa kiasi kwamba alishindwa kusema chochote". Baadae alikwenda hospitali na akamueleza daktari wake kwamba yupo katika umbile asilostahili."Nilikuwa na wasiwasi kwa mara ya kwanza na nilishindwa kutengeneza maneno ya kumwambia daktari,lakini nilimwambia nataka kuwa mwanamke,na alinambia sawa"
Katika mabadiliko makubwa mengine ya maisha yake, yalikuja septemba mwaka jana wakati alipoamua kutoka katika dini yake na kuwa muislamu.Anasema alivutiwa na uislamu kwa namna unavyohimiza,kujali na kuleta amani katika mafundisho yake kuliko dini nyingine."Nilikuwa na fikra juu ya jambo hilo(la kusilimu) kwa muda mrefu lakini ilikuwa kama mwiko kusilimu (kwa imani yake ya zamani)" alisema. Baada ya kusilimu anasema amepata mabadiliko makubwa katika nafsi yake. "Nilijisikia vizuri na nikawa na kitu cha kuamini (uislamu)na mwishowe nilihisi furaha na faraja ambayo sikuwahi kuipata katika maisha yangu"alisema.
Kabla ya kusilimu alizitafiti dini za budha na uyahudi,"Nilikuwa natafuta muelekeo sahihi wa maisha, naupenda (uislamu) ni mzuri na amani"kusilimu kwake kulikuja katika kipindi cha kiangazi kilichopita na aliolewa na Bwana Murad katika sherehe ndogo iliyofanyika huko London nyumbani kwa Murad.Akielezea mahusiano yake ya kindoa na mumewe anasema,"Nampenda, ni mkarimu na mtu mwenye maneno matamu,nilimuona mara mbili toka Tulipooana,wakati tulipofanya jimai"
Alipoulizwa je wakati bwana Murad anamuoa alikuwa akijua historia yake ya nyuma,alijibu kwa kusema, "sikumwambia kwamba nilibadili jinsia lakini lazima alikuwa na wasiwasi alipoona makovu yangu"
Hata hivyo Lucy ameingia katika matatizo na msikiti wake aliokuwa akiutumia wa Swindon, Wiltshire,ambapo wamemzuia kusali na wanawake wengine.Anasema amefanywa muhanga na waumini ambao walimuuliza historia yake na kisha kumzuia kwa sababu amebadili jinsia na kwamba hatakiwi kusali pamoja na wanawake kwani yeye ni mwanaume."Walisema nisisali na wanawake kwani mimi ni mwananaume,niliwaambia mimi ni mwanamke na nikaondoka zangu."
Pia amewalalamikia polisi kwa kutokuchukua hatua zozote kwa kubaguliwa kwake.Kwa sasa Lucy anataka kujua haki yake juu ya hukumu ya mtu aliyebadili jinsia katika uislamu.Aidha analalamikia waumini kwamba wanamchukulia katika namna isiyopendeza na kumnyanyapaa, "Wananiuliza maswali kuhusu saizi ya sidiria ninayovaa,kuhusu ukubwa wa koromelo,siku zangu za hedhi,na kutaka kuona cheti changu cha kuzaliwa" alilalamika na kuongeza, "Natumaini watu watabadili mienendo yao ili watu wengine kama mimi tuweze kuwa huru".Ingawa hasali katika msikiti huo, anaendelea kufanya ibada nyumbani kwake na anajifunza masuala mbalimbali ya dini na Quran.
Akizungumzia madai ya Lucy kuzuiwa kusali,msemaji wa msikiti huo amesema hajazuiwa kusali bali asali sehemu ya wanaume na si vinginevyo.Alisema, "Layla alijiunga katika darsa letu la kinamama mwishoni mwa mwaka jana,kwa nia ya kujifunza kiarabu."
"Hakuwa anajua kabisa kiarabu wakati anajiunga na darsa letu lakini miezi michache alikuwa na maendeleo mazuri.Alishirikiana na wana darsa na wanawake wote mpaka alipoondoka mwezi Juni mwaka huu,hatukujua kama alifanya mabadiliko ya jinsia."
Msemaji huyo aliongeza Kwamba Layla hakuweka wazi mabadiliko ya jinsia yake wakati wa kujaza fomu ya kujiunga na darsa.Na walianza kuhisi kuna anachoficha baada ya kutaka kuolewa kwani hakuonesha furaha pale alipotakiwa kuwasilisha vielelezo vya utambulisho wake. "Kwa bahati mbaya,hakuwa na furaha ya kuwasilisha hati yake kama vile pasipoti au cheti cha kuzaliwa kama sehemu ya mchakato wa ndoa yake" aliongeza msemaji huyo.
Anasema Layla hukuweza kufanya hivyo na badala yake akatumia njia ya kulalamika kwamba mwalimu wake wa kujitolea amemnyanyasa kwa kumuuliza maswali ya kumdhalilisha kama siku zake za hedhi na ukubwa wa matiti yake, na baada ya darsa Layla alimtumia mwalimu wake meseji za vitisho.Baadae palifanyika kikao na mwisho Layla aliomba msamaha na kusema anaondoka kwenda London kwa ajili ya kuolewa.Layla alisema kwamba cheti au pasipoti si muhimu katika ndoa ya kiislamu na kwamba msikiti hauna haki ya kuthibitisha kama yeye ni mwanamke au mwanaume
Lucy ambaye alifanyiwa operesheni huko London, pia aliwahi kufanya kazi katika wizara ya ulinzi kama mbeba mizigo ya jikoni.
Habari kwa hisani ya ahbaabur.blogspot.com

![]() |
| Lucy kushoto akiwa na kaka yake Soren (aliye kulia) |
![]() |
| Msikiti wa swindon alipokuwa akisali |
Saturday, 7 September 2013
AL-WAFD: RAIS OBAMA NI MWANACHAMA WA SIRI WA IKHWANUL MUSLIMIN
Shadi Hamid ameviambia vyombo vya habari vya Misri kwamba Rais Barack Obama ni mwanachama wa Ikhwanul muslimin kwa muda mrefu.Taarifa hiyo iliyokuja kwa njia ya Twitter na pia kupitia katika kurasa za mbele za magazeti ya Misri,imezua mjadala mkubwa kwa wafuatiliaji wa siasa za kimataifa.
Aidha Shadi alisema ndani ya habari hiyo kwamba Khairat al Shafer ambaye ni mtoto wa kiongonzi wa kikundi cha Ikhwanul Muslimin,aliwahi kumtisha Rais Obama wa Marekani kwamba atatoa nyaraka zinazoonyesha uwanachama wa Rais wa huyo katika kikundi cha Ikhwanul Muslimin. Taarifa hiyo inasema kwamba Obama alivutiwa na Ikhwanul Muslim wakati alipokuwa akiishi nchini Indonesia.
Ukiachana na tuhuma hizo zinazomkabili Rais Obama kuhusu uwanachama wake katika kikundi hicho,habari kwenye gazeti la Al-Wafd zimeeleza kwamba Malik Obama ambaye ni kaka wa rais Obama wa Marekani anahusishwa na uwanaharakati wa kikundi cha Al-Qaeda.
Wakati huo huo,Jonathan Spyer mwenye asili ya kiarabu ambaye ni kiongozi mwandaminzi wa kituo cha utafiti cha Global International Affears amelilalamikia gazeti la Al-Wafd kwamba ndilo ambalo limemtuhumu moja kwa moja rais Obama kuwa mwanachama wa Ikhwanul Muslimin.
Jonathan Spyer anaamini kwamba madai hayo yamejikita kwa kule kutokuridhishwa na sera za Obama pale alipo kataa kuelezea ukosolewaji wa Morsi na Chama chake cha Ikhwanul muslimin.Wote ambao hawamkubali Morsi na serikali yake iliyoondolewa madarakani na jeshi la nchi hiyo,wanamuona Obama ni mfuasi mzuri wa Morsi na Ikhwanul Muslimin.
Kwa mujibu wa Spyer anasema wamisri wanaamini Obama amekosa busara za kustaajabisha na tabia isiyo nzuri dhidi ya Ikhwanul Muslimin ambapo kwa dhati wanaamini kunasababishwa na hofu ya ufichuliwaji wa siri ya uanachama wake katika kikundi hicho.
Taarifa zinaelezea kwamba vyombo vya habari vya Misri havina mipaka linapokuja suala la ukosolewaji wa rais Obama wa Marekani.
Habari kwa hisani ya ahbaabur.blogspot.com
![]() |
| Gazeti la Al-Wafd la 30 august,2013 |
![]() |
| malik obama na barack obama,oktoba 3,1992.Katika harusi ya obama ambapo malik alikuwa bestman wa obama |
Friday, 6 September 2013
WAANDAMANA KUPINGA MISS WORLD,INDONESIA
Maelfu ya waandamanaji wamejitokeza mwanzoni mwa wiki hii kupinga mashindano ya Miss World yanayotarajia kuanza jumapili ya kesho nchini Indonesia .Waandamanaji hao wametaka shindano hilo lifutwe kwani linadhalilisha utu wa mwanamke na ni kinyume na mafundisho ya kiislamu.
Upinzani mkubwa toka kwa waandamanaji hao umezidi, katika taifa hilo lenye Waislamu wengi zaidi duniani,licha ya waandaaji kudai wameondosha vazi la ufukweni (bikini)
Baadhi ya wanaume na wanawake 800 kutoka kundi la Hizbut Tahrir la Indonesia wamekusanyika katika mji wa Jakarta nje ya wizara ya ustawi wa jamii, wakitoa wito kwa serikali wa kufuta shindano hilo.
Aidha waliandamana hadi makao makuu ya shirika la habari la Indonesia MNC kwamba liache kutangaza habari za shindano hilo lililopotoka. "Je, tunataka nchi yetu kuonekana kama ya watu wa ngono?" mmoja wa waandamaji alisema kwa sauti kubwa .
"Sisi tutaendelea kuandamana na kuwaambia watu jinsi ya udhalilishaji wanawake kwa kufanyika shindano hili," alisema mratibu wa maandamano hayo, Zikra ASRI,huku akiwa amezungukwa na wanawake waliovaa hijabu nyeupe na baibui nyeusi.
Mjini Medani katika kisiwa cha Sumatra, wanachama 500 wa Hizbut Tahrir waliandamana hadi majengo ya serikali, na kudai kuwa shindano hilo lifutwe.Licha ya upinzani kuongezeka , waandaaji wamesema kuwa shindano hilo lazima lifanyike na halita athiri heshima na utamaduni wa indonesia
Shindano la Miss Dunia linatarajiwa kuanza Jumapili katika kisiwa cha Bali, na mshindi anatarajiwa kupatikana katika jiji la Jakarta Septemba 28.
Nchi hiyo yenye watu milioni 240,June mwaka jana mwanamuziki Lady Gaga alilazimika kufuta onesho lake,baada ya viongozi wa dini ya kiislamu kutishia kuchoma moto ukumbi ambao atafanyia onesho hilo,baada ya mwanamuziki huyo kuonesha mavazi yake ya ndani.
Habari kwa hisani ya ahbaabur.blogspot.com
Habari kwa hisani ya ahbaabur.blogspot.com
![]() |
| waandamanaji nchini indonesia |
Subscribe to:
Posts (Atom)